Azam F.C na hesabu mpya dhidi ya Tanzania Prisons

Azam F.C na hesabu mpya dhidi ya Tanzania Prisons

BAADA ya kugawana pointi moja wakiwa ugenini mbele ya Lipuli FC, kikosi cha Azam FC kimeanza kujiandaa kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Alhamisi uwanja wa Sokoine.


Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Manganga amesema kuwa kupata poiinti moja ugenini ni hatua nzuri ambayo inawafanya wajipange upya kwa ajili ya michezo inayofuata.

Azam FC walionyesha ukomavu wao kwenye mchezo huo wa ugenini kwani walifungwa kipindi cha kwanza na Lipuli FC ambao waliamini matokeo yatakuwa hivyo mpaka mwisho.

BAO la Salimu Abdallah dakika ya 80 lilitibua mipango ya Lipuli na kuwafanya wagawane pointi moja Uwanja wa Samora, Iringa.

Azam FC wanashika nafasi ya pili wakiwa wamecheza michezo 22 wana pointi 49 huku kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 58.

Leave a Comment