breaking news New
Athanasi Mdamu ndani ya Kariobangi Sharks

Athanasi Mdamu ndani ya Kariobangi Sharks

Mshambuliaji wa Singida United, Athanasi Mdamu amesaini mkataba wa miaka mitatu kujiunga na klabu ya Kariobangi Sharks ya Kenya.

Mkurugenzi wa Singida United, Sanga Festo amesema kwamba Mdamu amesaini mkataba wa kujiunga na klabu hiyo ya Kenya kwa ridhaa ya uongozi wao.

Sanga amesema kwamba Kariobangi Sharks imemsajili Mdamu baada ya kumuona kwenye michuano ya SportPesa Super Cup mwezi uliopita mjini Dar es Salaam na kuvutiwa na uwezo wake.

Viongozi wa Sharks waliwasiliana na Klabu yetu na baadaye tukamruhusu mchezaji huyo aende akaongeze maarifa kwenye soka kwa manufaa yake na Taifa letu,”amesema Sanga.

Baada ya Athanas kwenda Kenya, tunategemea mchezaji mwingine kuondoka siku za karibuni kwenda kucheza barani ulaya na taratibu zake zote zimeshakamilika,” ameongeza Sanga.

Hii ni mwendelezo wa program ya Singida United kuwaruhusu wachezaji kwenda kucheza soka nje ya nchi pale tu wanapopata timu kama ambavyo mkataba wa timu na mchezaji unavyoeleza.

Leave a Comment