Ali Kiba wa Coastal Union ni tofauti sana

Ali Kiba wa Coastal Union ni tofauti sana

MAISHA anayoishi straika wa Coastal Union na msanii wa kimataifa, Ali Kiba ‘King Kiba’ akiwa mkoani Tanga ni ya kawaida kiasi kwamba wanaomzunguka ndio wanaojishtukia kuona wapo na msanii mkubwa.

Pamoja na ustaa alionao, King Kiba alikuwa anayafuata kikamilifu maelekezo ya kocha wake Juma Mgunda pamoja na kushirikiana na wachezaji wenzake katika mazoezi hayo.

Ni tofauti na namna ambavyo mashabiki walikuwa wanamuona ni mtu adimu na watofauti mpaka kufikia hatua ya kumuita mfalme wa Tanga, King Kiba alikuwa anajishusha na kujiona yupo sawa nao muda wote akiwaonyesha tabasamu, huku akiwapungia mikono ishara ya kuwasalimia.

Licha ya kuja na usafiri wake mazoezini na wakati wa mechi, hakukumfanya ajione yeye yupo juu ya wengine alikuwa anafuata utaratibu anapoambiwa na kocha wake Mgunda.

King Kiba anavyoizungumzia Coastal Union “Kikubwa ni sisi wachezaji kujituma na kupambana kadri tutakavyoweza ili kuhakikisha timu yetu inakuwa kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi.

Anasema.

“Ligi ni ngumu ila juhudi zetu ndizo zitakazotufanya tufikie malengo yetu kwa msimu huu ambao una mzunguko mrefu kutokana na uwepo wa timu 20,”

Leave a Comment